Home » » Wananchi hararini kukabiliwa na njaa

Wananchi hararini kukabiliwa na njaa

Written By Koka Albert on Monday, March 12, 2012 | 2:08 AM

Anthony Mayunga,Bunda
WAKAZI wa Kijiji cha Migungani, Kata ya Migungani katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, wanakabiliwa na tishio la njaa baada ya mazao ya mpunga kuathiriwa na maji yanayodaiwa kuwa na sumu yaliyotiririshwa na kiwanda cha Bundaa Oil Mill.

Kukauka kwa mazao hayo ambayo wanategemea kwa  biashara na chakula kumesababisha baadhi ya wananchi kuomba serikali  kuandaa utaratibu wa kuwapatia chakula cha msaada.

Uchunguzi wa Mwananchi katika mashamba ya wananchi, umebaini kuwa mazao yote yaliyoingiwa na maji ya sumu, Novemba 6, mwaka 2011 yameungua na wakulima hawakuweza kuvuna chochote.


Pia madhara ya maji hayo yanaonekana kuwa makubwa zaidi kwa kuharibu ardhi hiyo ambayo wanayoitegemea kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Maswi Chogo mmoja wa waathirika na maji hayo  alisema ana ekari tano za mpunga ambazo,  ziliaharibiwa na maji hayo na kufidiwa Sh25,000 za kununua mbegu.

“Unanunua mbegu kupanda wapi maana ekari hizo nilitegemea kupata zaidi ya magunia 100 ya mpunga sasa unapewa hela ya kununua debe moja upande kwenye ardhi ambayo imeharibiika,serikali inahusika kutuhujumu
sisi kwa kushirikiana na mwekezaji kweli?”alihoji kwa ukali akiwa shambani kwake.

Alisema wao wanatembea wamekufa kwa kuwa maji ya kunywa,kuoga, mifugo na mazao wanayokula yamekuwa yakichafuliwa na  maji ya sumu ambayo hutiririshwa.

Kichere Gikaro alisema zaidi ya ekari 55 zilichafuliwa na maji hayo mwishoni mwa mwaka jana, lakini alipewa Sh1 milioni kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa kata hiyo na kwamba fedha zilizowafikia wakazi 25 kwa ajili ya kununua mbegu ni Sh875,000.

Uchunguzi zaidi wa Mwananchi umebaini bei ya mchele katika soko la Bunda imepanda kutoka Sh 1,800 mpaka Sh2,300 kwa kilo moja tofauti Wilaya ya  Serengeti ambako kilo moja inauzwa Sh2,000.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger