Home » » Aliyekaribishwa Ikulu ampa JK sharti la kupanda mlima

Aliyekaribishwa Ikulu ampa JK sharti la kupanda mlima

Written By Koka Albert on Thursday, March 15, 2012 | 2:26 AM

Salum Maige,Geita
SAKATA la muhubiri na muumini wa Kanisa la Kibaptist lililopo Wilayani Geita la kufunga bila kula kwa muda usiojulikana akifanya maombi kwa ajili ya Rais Jakaya Kikwete na Tanzania limechukua sura mpya baada ya muhubiri huyo kutoa siku 20 kwa Kikwete awe amefika kwenye mlima alioweka kambi kabla ya kushuka.

Muhubiri huyo alitishia kuwa iwapo hatafika mambo yatakayolikumba nchi, asilaumiwe.

Muhubiri huyo Mussa Lunyeka (35) mkazi wa Kijiji cha Chabulongo, Kata ya Bung’hwangoko, Kasamwa, amekuwa akiendesha maombi yake mlimani kijijini hapo kwa madai kwamba  Mwenyezi Mungu amemwambia afanye hivyo.

Kwa mjibu wa Lunyeka ambaye yuko kwenye kilima hicho tangu Feburuary 7, mwaka huu alisema kupitia maombi hayo, amemtaka Rais Kikwete afike kwenye kilima hicho kwa mazungumzo zaidi kuhusu  mstakabali wa nchi. Alisema maelekezo hayo alipewa na Mungu.

“Leo ni siku ya 29 niko hapa mlimani nimefunga kwa ajili ya kumwombea Rais wangu pamoja na nchi,  kuna mambo ambayo nimeelezwa na Mungu na ninapaswa kumweleza Rais kuhusu mwelekeo wa nchi yetu.

"Nikiwa hapa nimeoteshwa tena ndoto nyingine ikinitaka nishuke kweye kilima hiki Machi 30, mwaka huu na iwapo Rais kikwete hatafika hapa kwa siku 22 zilizobaki, naomba nisilaumiwe maana yatakayotokea hapa chini kwa mjibu wa ndoto yangu ni mambo mazito hivyo kabla hayajatokea namwomba Rais afike na kusikiliza niliyoelekezwa na Mungu.

“Maandiko yanasema kwamba katika kitabu cha Zaburi 33:3, "Niiteni nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua, unaweza kujifikiria kuwa Mungu amekusudia neema kwa Tanzania, yawezekana kuna watu hawapendi kuiona hiyo neema kwa Rais na hata kwa Watanzania,. Mungu ameniambia nipande kwenye mlima huu na kufunga kwa kufanya maombi, na kuna mambo ambayo Mungu anapaswa kuzungumza na Rais kupitia kwangu kwa hiyo anapaswa kuja hapa nilipo ili nimweleze mambo hayo muhimu sana,’’ alisema Lunyeka.

Mwaka jana muhubiri huyo alisafiri kwa baiskeli kutoka kijijini Chabulongo hadi Ikulu, Dar es Salaam kumpongeza Rais kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa mwaka 2010.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/21110-aliyekaribishwa-ikulu-ampa-jk-sharti-la-kupanda-mlima
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger