Home » » Kampuni zasambaza dawa bandia

Kampuni zasambaza dawa bandia

Written By Koka Albert on Tuesday, March 20, 2012 | 12:22 AM

Mustapha Kapalata,Nzega
WANANCHI wa Kata ya Shigamba wilayani Nzega, mkoani Tabora wameilalamikia kampuni ya Biosustain (T) LTD kwa kuwapatia dawa bandia za kupulizia pamba tofauti na makubaliano ya awali.

BIOSUSTAIN ni kampuni inayojihusisha na kilimo cha pamba cha mkataba wilayani hapa yenye makao makuu yake mkoani Singida
Wananchi hao kwa nyakati tofauti walisema dawa hiyo aina ya Zetabestox,  haina uwezo wa kuangamiza wadudu na kwamba wadudu wanaendelea kushambulia mazao.

Kampuni hiyo imesambaza chupa za dawa bandia zaidi ya 1,017 huku kila chupa ikiuzwa Sh1,500 na kampuni hiyo ina hudumia Kata 34 wilayani hapa.

Daudi Nhonge Diwani wa kata hiyo alisema kuwa kampuni hiyo imesababisha hasara kubwa kwa wananchi hasa katika msimu huu wa kupulizia dawa kwenye zao la pamba.

Diwani huyo alishauri taratibu zifuatwe kama mkataba unavyoeleza kwamba endapo  mkulima au kampuni atakaye sababisha hasara anapaswa kuchukuliwa  hatua za kisheria.

‘’Kampuni ya Biosastain imewapa hasara kubwa wananchi hasa kwa kuwapatia dawa bandia, tunaiomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya ubadhilifu huo,’’ alisema diwani huyo.

Zaidi ya fekati 2,500 za pamba zimeliwa na wananchi hao kutokana na kampeni kubwa iliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Florence Holombe.

Ofisa Kilimo na Mifugo, Willam Mafwele akizungumza kwa njia ya simu yake ya mkononi alisema amepokea  malalamiko ya wananchi kuhusu dawa hiyo na kufafanua kwamba tayari ameitaarifu bodi ya pamba.

 Naye Yohana Basanda Msimamizi wa kampuni hiyo akizungumuza kuhusu malalamiko hayo alikiri kwamba dawa hiyo haiui wadudu na alisisitiza kuwa wanafanya jitihada za kupata dawa nyingine.

Basanda aliwaomba wakulima waendelee kusubiri kwa kuwa tatizo linatafutiwa ufumbuzi haraka.Alisema kampuni iliwauzia dawa bandia na tayari wamepeleka taarifa kwa kampuni hiyo kwamba wamepokea malalamiko kutoka kwa wananchi dawa hiyo haifanyi kazi
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger