Home » » Polisi akutana na kichapo kutoka kwa mhalifu

Polisi akutana na kichapo kutoka kwa mhalifu

Written By Koka Albert on Saturday, March 31, 2012 | 11:23 PM

Julieth Ngarabali, Kibaha
POLISI mmoja kati ya watatu waliokuwa kwenye doria, amepigwa na kujeruhiwa na mtuhumiwa walipokwedna nyumbani kwake (mtuhumiwa) kumkamata.

Tukio hilo lilitokea saa 1:00 usiku wa kuamkia jana Mtaa wa Mbagala Mlandizi, wilayani Kibaha, mtuhumiwa aliyempiga askari huyo anadaiwa kulawiti alifuatwa kupelekwa kituoni cha polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema askari aliyejeruhiwa ni E. 4420 Sajini Dady, huku mtuhumiwa akitajwa kuwa ni mkazi wa Mbagala, Mlandizi.

Mangu alisema wakati wa ukamataji huo, mtuhumiwa alikataa kutii sheria na kusababisha vurugu zilizopelekea kumjeruhi kichwani polisi kwa kitu chenye ncha kali.

Alisema askari aliyejeruhiwa alipelekwa Hospitali Teule ya Tumbi, alipatiwa matibabu na kuruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.

Hata hivyo, polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituoni na kwamba, zaidi ya kulawiti amefunguliwa kesi nyingine ya kumjeruhi askari wakati akitekeleza majukumu yake.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger