Home » » Asilimia 35 ya wangonjwa wa kansa ni wa sigara’

Asilimia 35 ya wangonjwa wa kansa ni wa sigara’

Written By Koka Albert on Tuesday, March 20, 2012 | 12:20 AM

Tausi Ally                                
UVUTAJI sigara au wanaopokea moshi wa sigara wametajwa kulazwa wengi kwa kansa nchini.Habari ziolisema asilimia 35 ya watu wanaougua ugonjwa wa kansa waliolazwa Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, wamepata ugonjwa huo  baada ya  matumizi ya sigara (tumbaku) au kupokea moshi wa sigara kutoka kwa wavutaji.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Hospitali ya IMTU, Dk  Ali Mzige wakati akichangia mada kwenye mkutano wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) wa kuzuia matumizi ya sigara, tumbaku, ugoro, kuberi na bangi.

Dk Mzige alisema matumizi ya vilevi  hivyo kwenye jamii katika mikusanyiko ya watu hususani kwenye vituo vya afya,  yanasababisha madhara kwa wavutaji na kwa wale wasiovuta, lakini wanapokea moshi kutoka kwa wavutaji. "Asilimia 85 ya kansa wanazoumwa wanaume duniani vyanzo vyake vinahusishwa na  matumizi ya tumbaku, sigara, ugoro, kuberi  na kwa wale wasiotumia kupokea moshi kutoka kwa watumiaji hao,"alisisitiza Dk Mzige.

Alisema watumiaji wa sigara na tumbaku wapo katika hatari ya kupata madhara  ya nywele  kunyonyoka,  mtoto wa jicho, kukunjamana kwa ngozi, kutosikia vizuri na saratani ya ngozi.

 Madhara mengine wanavyoweza kuyapata watumiaji hao ni  meno kuoza, mapafu  kushindwa  kufanya kazi vizuri,  ulaini wa mifupa, magonjwa ya moyo, vidonda vya tumbo,  vidole kubadilika rangi, kansa ya kizazi, kuharibika kwa mimba,  kupunguza nguvu za kiume, ukurutu, kuziba kwa mishipa midogo ya damu  pamoja na kansa ya mapafu na viungo vingine.

 “Madhara yanayotokana na matumizi ya sigara na tumbaku ni makubwa, tushirikiane kuzuia matumizi ya vitu hivi kwenye mikusanyiko ya watu na hata kwenye vituo vya afya  kwa sababu, takwimu zinatisha na wanaothirika zaidi ni wale wasiotumia vilevi hivyo bali wanapokea moshi tu,” alisisitiza kusema Dk Mzige.

 Alibainisha kuwa watu wengi wanaojihusisha na matukio ya kujiua, ukifuatia undani wao walikuwa ni wavuta sigara ambapo kwa upande wa bangi Dk Mzige alisema inasababisha ungonjwa wa kansa na  kuharibu ubongo kwakuwa ina kemikali 400.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger