Home » » ‘Mfumuko wa bei (Inflation) umepungua’

‘Mfumuko wa bei (Inflation) umepungua’

Written By Koka Albert on Thursday, March 15, 2012 | 11:53 PM

Ibrahim Yamola
MFUMUKO wa bei nchini katika kipindi cha mwezi uliopita ulipungua, kutoka asilimia 19.7 Januari mwaka huu hadi kufikia asilimia 19.4

Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,  Dk Albina Chuwa, kupungua kwa mfumuko wa bei  katika kipindi hicho kunamaanisha kuwa kaasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma,  imepungua.
“Mfumuko wa bei ya vyakula na vinywaji baridi, ulipungua hadi kufikia asilimia 26.7 Februari mwaka huu kutoka asilimia 27.8 Januari,” ilisema taarifa hiyo.Ilisema mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula majumbani  katika migahawa  ilipungua hadi kufikia asilimia 25.5  ikilinganishwa na asilimia 26.2  Januari mwaka huu.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa kasi ya ongezeko kwa bidhaa zisizo za vyakula ilibaki kuwa asilimia 11.8 Februari mwaka huu  kama ilivyokuwa Januari.
“Mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa Februari mwaka huu ulipungua hadi kufikia asilimia 8.6 kutoka asilimia 9.0 Januari mwaka huu,” ilisema.Taarifa hiyo ilisema hata hivyo mfumuko wa bei katika nishati uliongezeka hadi kufikia asilimia 33.5 mwezi uliopita ikiinganishwa na asilimia 30.1 Januari.

 Ilisema mfumuko wa bei wa nishati umesababishwa na kuongezeka kwa bei za umeme kwa asilimia 36.7.
 “Kundi la nishati na mafuta limeonyesha pia kuwa na mwenendo wa bei ya taifa usio imara ikilinganishwa na makundi mengine kwa kipindi husika” ilisema taarifa hiyo.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger