Home » » Serikali itukumbuke vijana

Serikali itukumbuke vijana

Written By Koka Albert on Thursday, March 15, 2012 | 2:42 AM

NIKIWA kijana mwenye ndoto za kufanikiwa maishani, naishauri Serikali iwekeze kwa vijana nchini. Nasema hivi kwa sababu sisi tuna nguvu ya kuzalisha mali na kulijenga Taifa.

Ombi langu kwa Waziri wa Michezo, Utamaduni na maendeleo ya vijana atusaidie vijana, hasa sisi tunaojishughulisha na shughuli  zisizo rasmi .

Kazi zetu zirasimishwe na tuingizwe kwenye mfumo wa mafao ya uzeeni inayosimamiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Vijana tunajishughulisha mno lakini kwa kuwa kazi zetu hazitambuliki, tunashindwa kuendelea. Tunaajiriwa kama vibarua, lakini kwa kuwa hatuna ajira, haki zetu hupotea bure pale tunapoachishwa kazi.

Uwezo wa kusimama mahakamani na matajiri wenye fedha hatuna, matokeo yake ni kudhulumiwa tu.
Nasema hivi nikiwa na uhakika kuwa kuna watu hadi sasa wamezeeka wakifanya kazi za vibarua, lakini hawajafaidika, wanaendelea kuteseka tu.

Vilevile Serikali itusaidie vijana kupitia sekta ya kilimo. Kama ardhi ya kutosha ipo na vijana tupo, kwa nini tushindwe kuendelea?
Serikali ituwezeshe kupata pembejeo na masoko ili tuweze  kufaidika na kilimo.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger