
Na Shija Felician
KWA muda mrefu, mkoa wa Shinyanga umekuwa ukishika mkia katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba.
Kwa mfano, takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, zinaonyesha mkoa huo ulishika nafasi ya mwisho katika miaka ya 2008 na 2009.
Hata hivyo, matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa mwaka 2011 ulikuja na sura tofauti hasa baada ya mkoa huo kutoa shule kinara wa mtihani huo na hata wanafunzi bora kitaifa.
Shule iliyoupandisha chati mkoa wa Shinyanga inaitwa Kwema ambayo ni shule ya mchepuo wa Kiingereza iliyopo wilayani Kahama.
Kwa mujibu wa taarifa za matokeo ya mtihani huo zilizotolewa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), shule ya Kwema ilitajwa kuwa ya pili kitaifa kati ya shule 15,510, huku pia ikitoa wanafunzi bora wa kwanza, wa tatu na wa nne kitaifa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shule hiyo, Pauline Mathayo, siri kubwa ya kufanya vizuri kwa shule yake ni ari kubwa ya kufundisha waliyo nayo walimu anaosema aghlabu humaliza silabasi muda mrefu kabla ya mitihani ya mwisho,jambo linalowapa fursa ya kuwapa mazoezi ya kutosha wanafunzi.
“Tuna walimu waliobobea na wenye nia ya kujituma katika kuelimisha wanafunzi. Pia wazazi wanashirikiana bega kwa bega na uongozi kuhakikisha wanafunzi wanapata mahitaji yao ya shule kwa wakati,’’anasema
Tofauti na hali Ilivyo katika shule nyingi hata zile kongwe na maarufu anajivunia kuwa na walimu zaidi ya 70 wanaowafundisha wanafunzi 1600 waliopo shuleni hapo.
Anasema ufaulu mzuri wa shule yake ni faraja kwa mkoa wa Shinyanga, huku akisema mkoa huo sasa umeamka kielimu.
Anaeleza kuwa tangu shule yake ianze kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2002, hakuna mwanafunzi aliyefeli, huku wote wakichaguliwa kujiunga na shule za sekondari.
Kauli za wanafunzi
Innocent Nyakabunda ndiye aliyeongoza jahazi la ufaulu wan shule yake kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa.Unapozungumza naye kwa haraka utagundua kuwa mtoto huyu anajiamini na ana upeo mkubwa ndani yake.
Post a Comment