Home » » Ufafanuzi wa NECTA haukubaliki

Ufafanuzi wa NECTA haukubaliki

Written By Koka Albert on Wednesday, March 21, 2012 | 7:16 AM

Dk. Joyce Ndalichako

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, kwa mara nyingine ametetea uamuzi wa baraza lake kuwafutia matokeo ya mtihani wa kidato cha IV baadhi ya wanafunzi. Nimesikia kwa umakini utetezi alioutoa.

Kimsingi Dk. Ndalichako ameeleza mambo matatu makubwa kuhalalisha kile alichoita, “kukithiri kwa vitendo vya udanganyifu katika vyumba vya mitihani.”

Kwanza, Dk. Ndalichako amesema baraza lake limelazimika kuchukua hatua hiyo ngumu baada ya baadhi ya walimu na wasimamizi wa mitihani kushiriki katika “uchafuzi wa mitihani.”

Pili, amasema baadhi ya wanafunzi walikutwa na majibu ya mitihani kupitia simu zao za mkononi.
Tatu, amesema wasimamizi walikamata vikaratasi ambavyo wanafunzi walikuwa wanavitumia “kupasiana” majibu.

Lakini kabla ya Necta kubebesha tuhuma wasimamizi wa mitihani sharti ieleze kama katika mtihani huu, ilibadilisha mfumo wake wa kuteua wasimamizi waaminifu kama wanavyofanya siku zote.
Hii ni kwa sababu, wengi wa wasimamizi ni wale wale waliowahi kutaka kutunikiwa tuzo kutokana na kulipatia sifa nzuri ya “usimamizi wenye tija,” baraza lake.

http://www.mwanahalisi.co.tz/ufafanuzi_wa_necta_haukubaliki
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger