Home » » ‘Mfumuko wa bei unaweza kukimbiza wawekezaji’

‘Mfumuko wa bei unaweza kukimbiza wawekezaji’

Written By Koka Albert on Saturday, March 31, 2012 | 11:32 PM




MFUMUKO wa bei unaweza kuwakimbiza wawekezaji wanaotaka kuja nchini kuwekeza rasilimali zao kama  utaendelea kukua kama ilivyo sasa.Kwa sasa kiwango cha mfumuko wa bei, kimefikia asilimia 19.

Tahadhari hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered, Jeremy Awori, alipokuwa akiwasilisha mada yake katika semina ya Mameneja wa Rasilimali Watu kutoka kampuni mbalimbali.

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuangalia masuala mbalimbali ya rasilimali watu iliandaliwa na Chama cha Wanataaluma ya Rasilimali Watu Tanzania.

Awori alisema tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania ndiyo yenye mfumuko mkubwa wa bei miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, jambo linaloweza kuathiri biasharana za uwekezaji.“Mfumuko wa bei ukiwa juu mwekezaji analinganisha na nchi nyingine akiona kule hakuna mfumuko mkubwa anajiuliza kwanini niwekeze hapa ambapo itanigharimu sana wakati kuna nchi mfumuko uko chini na anaweza kufanyabiashara vizuri, maana mfumuko wa bei unasababisha gharama kubwa hata unapoajiri watu,” alisema.

Pia alisema Tanzania ina fursa ya kukuza uchumi wake kwa kiwango kikubwa hasa ikizingatiwa kuwa imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi kuliko nchi nyingi za Afrika.Alisema Tanzania ina madini mengi na maliasili nyingi ambazo hazipatikani katika nchi nyingi na kwamba hiyo  ni fursa kubwa ya kuwezesha uchumi kupaa kwa haraka.

“Kuna vitu vingine huhitaji kuambiwa, hivi nani asiyejua kuwa Tanzania imejaa madini na maliasili za kutosha, tukivitumia hivi vizuri inaweza kuwa njia ya kutosha kuondokana na hali iliyopo sasa,” alisisitiza.Awori alisema biashara kati ya Tanzania na mataifa makubwa kama China, inaongezeka na kwamba kuna haja kwa wanataaluma kuichukua hiyo kama fursa kwao.

Alitoa mfano kuwa Wachina wengi wanakuja Tanzania kuendesha miradi mikubwa katika sekta mbalimbali kama ujenzi na kwamba wanahitaji huduma mbalimbali kama za kibenki.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger