Home » » Mwanafunzi aongezwa Twiga Stars

Mwanafunzi aongezwa Twiga Stars

Written By Koka Albert on Monday, March 26, 2012 | 5:03 AM

Vicky Kimaro
KOCHA wa Twiga Stars, Boniface Mkwasa amemuongeza mshambuliaji Rehema Salum wa Shule ya Sekondari Lord Baden ya mkoani Pwani kwenye kikosi chake kitakachoingia kambini kambini Machi 25.

Akizungumza jana, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bonifance Wambura alisema Rehema aliibuka mfungaji bora kwenye mashindano maalumu ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoshirikisha shule nane za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na kumalizika Machi 8.

Alisema Twiga Stars itaingia  kambini kwenye kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Ruvu mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Fainali za Wanawake Afrika (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

Timu hiyo itacheza na Ethiopia kusaka tiketi ya kwenda Equatorial Guinea, ikianzia ugenini Addis Ababa kwa mechi itakayochezwa Mei 26 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam.
Katika raundi ya kwanza, Twiga Stars iliitoa Namibia kwa jumla ya mabao 7-2. Ilishinda ugenini 2-0 na kuibuka na ushindi mnono nyumbani wa mabao 5-2.

Machi 10 mwaka huu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara alizindua akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ili ishiriki vyema michuano ya AWC.
Wambura alisema wachangiaji wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389, ambapo kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala mmoja ni sh500,000. Katika uzinduzi huo, Mukangara alichangia sh. milioni moja.

Wakati huohuo, Wambura alisema mtihani kwa kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji na mechi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) utafanyika Machi 31 kwenye ofisi za TFF. Alisema kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili, ambapo watapewa kanuni mbalimbali za Fifa na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo.
Katika mtihani wa awali uliofanyika hivi karibuni, mawakala 13 walishiriki lakini hakuna aliyefaulu.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger