Home » » Majambaziyamvamia Mbunge Maji Marefu

Majambaziyamvamia Mbunge Maji Marefu

Written By Koka Albert on Monday, March 5, 2012 | 10:46 PM


Burhan Yakub,Tanga
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani ‘almaarufu Profesa Majimarefu’, usiku wa kuamkia jana alivamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi  katika eneo la Mombo, walipoweka mawe barabarani kwa lengo la kuteka magari.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini hapa, Profesa Majimarefu alisema tukio hilo lilitokea saa 7:00 usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo alipopita wakati akitokea jijini Nairobi kuelekea Tanga
kwenye mkutano wa wadau wa mkonge uliofanyika jana kwenye jijini hapa.

Akielezea tukio hilo, mbunge huyo alisema kuwa wakati alipofika eneo hilo walikuta mawe yamepangwa barabarani na dereva wake alipoona hali hiyo aliingia kwenye mtaro kuyakwepa mawe hayo lakini wakiwa pembeni ya barabara, walitupiwa mawe ambayo yaliweza kuvunja kioo cha gari
upande aliokaa mbunge huyo.

“Tulipofika eneo hilo Hoteli ya Liverpool naiona ile pale, tukakuta mawe barabarani dereva wangu Omari alipoyaona akaingia pembeni kuyakwepa kule pembeni tulitaka kupinduka, lakini majambazi wale waliturushia
mawe yaliyovunja kioo,” alisema mbunge huyo huku akionyesha gari hilo kwa waandishi wa habari.

Akielezea zaidi alisema alitoka jijini Nairobi saa 12:00 jioni Jumapili kuelekea jijini Tanga kwenye mkutano huo lakini alipofika katika eneo la Manga –Kibaoni akiwa anaendesha yeye gari hilo lenye namba T 265 BLS aliamua kuweka gari pembeni ili wapumzike
kisha waendelee na safari.

“Tulilala pale kama dakia 20 hivi dereva wangu aliamka akasema mzee hatuwezi kulala hapa bora tusogee mbele maana tumeshafika Korogwe bora tukalale nyumbani kisha kesho (jana) twende Tanga mkutanoni, nilimkubalia kumbe tunakwenda ‘kwenye mtaji wa maskini’,” alisema
mbunge huyo.

Mbunge huyo alisema atahakikisha anashirikiana na wananchi wa eneo la Mombo kuhakikisha vijana wanaojihusisha na uhalifu na kuchafua sifa nzuri ya wakazi wema wa eneo hilo, wanakamatwa na kufikishwa
katika vyombo vya sheria.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema polisi wameanza kazi ya kuwasaka watu  waliofanya uhalifu ili waweze kuwakamata kutokana na vitendo hivyo.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger