Home » » Petroli, dizeli yapanda tena

Petroli, dizeli yapanda tena

Written By Koka Albert on Wednesday, March 7, 2012 | 6:10 AM

Geofrey Nyang'oro
MAMLAKA YA  Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza  bei mpya ya mafuta ambayo itawalazimisha watu kutumia fedha zaidi kununua petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Katika ongezeko hilo Ewura imeongeza zaidi ya shilingi 100 kwa aina tatu za bidhaa  hizo.Katika mabadiliko hayo ya bei, lita moja ya petroli sasa  imeongezeka kwa Sh153 sawa na asimilia 7.67, lita moja ya dizeli Sh119 sawa na asilimia 6.01 na mafuta ya taa Sh 104 kwa lita moja sawa na asilimia  5.35.  Sasa lita moja ya petroli itauzwa Sh2,144 kwa lita moja badala ya Sh 1,991, dizeli itauzwa Sh2,116 kwa lita badala ya Sh1,997 na mafuta ya taa Sh2,055 wakati bei badala ya Sh1,951 kwa lita.

Taarifa ya Ewura iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa  bei hiyo mpya ya mafuta inatarajia kuanza kutumika leo Jumatato.  "Mabadiliko haya ya bei za mafuta nchini yametokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia na kushuka kidogo  kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani," sehemu ya taarifa hiyo imefafanua.

Kwa mujibu wa Ewura thamani ya shilingi imeshuka kwa asilimia 0.13  ikilinganishwa na thamani ya shilingi katika toleo lililopita. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika kama ifuatavyo: 
Kwa mujibu wa Sheria ya mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. Pia Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

 Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.  "Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na Ewura ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 Desemba 23, mwaka jana," alifafanua taarifa hiyo. 
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger