Home » » Stars, Mambas zaingiza mil. 64.7/-

Stars, Mambas zaingiza mil. 64.7/-

Written By Koka Albert on Thursday, March 1, 2012 | 11:30 PM


MECHI ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), zilizopangwa kufanyika mwakani nchini Afrika Kusini, iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi, kati timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Msumbiji ‘Mambas’ imeingiza sh 64,714,000.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 16,776 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo, uliomalizika kwa Stars kulazimisha sare ya bao 1-1 na Msumbiji.

Wambura alisema sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani, ambako watu 14,403 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh 3,000 kwa kila mmoja.

Viingilio vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh 10,000 VIP C, sh 15,000 VIP B wakati VIP A iliyoingiza watazamaji 91, kiingilio kilikuwa sh 20,000.

Alifafanua kuwa mgawanyo wa mapato hayo, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ilikuwa sh 9,871,627, gharama ya kuchapa tiketi sh 4,500,000, malipo kwa waamuzi wanne na kamishna wa mchezo sh 12,180,000 huku ulinzi na usafi wa uwanja sh 2,350,000.

Makato mengine ni malipo kwa kampuni ya Wachina (Beijing Construction) sh 2,000,000, maandalizi ya uwanja sh 400,000 wakati asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh 6,682,475, asilimia 10 ya uwanja sh 3,341,237, asilimia 5 ya Shirikisho Soka Barani Afrika (CAF) sh. 1,670,136 na asilimia 65 ya TFF sh 21,718,042
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger