Home » » Viingilio Simba vs Kiyovu hadharani

Viingilio Simba vs Kiyovu hadharani

Written By Koka Albert on Thursday, March 1, 2012 | 11:29 PM


 
Benjamini Mkapa National Stadium

WAKATI wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), Simba ikitarajiwa kurejeana na Kiyovu ya Rwanda kwenye dimba la Taifa Jumapili, kiingilo cha chini kimepangwa kuwa sh 5,000.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatika jijini Dar es Salaam jana, kiingilio hicho kitahusisha mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani, ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kuhudhuria.
Taarifa hizo, zinaeleza kuwa kiingilio cha juu katika mchezo huo ni sh 30,000, ambacho kitahusisha mashabiki watakaokaa jukwaa la VIP A.
Aidha mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya chungwa watalipa sh 8,000, VIP C sh 20,000 na VIP B watalipa sh 15,000 .
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger