Home » » Tunaelekea wapi Jamani!!! Danguro la watoto la Ibuliwa Dar

Tunaelekea wapi Jamani!!! Danguro la watoto la Ibuliwa Dar

Written By Koka Albert on Friday, March 2, 2012 | 1:46 AM

GESTI moja maarufu (jina tunalo) iliyopo Buguruni Malapa, Dar es Salaam imegeuzwa danguro la watoto, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Katika msako wa kila siku unaofanywa na jeshi la polisi, gesti hiyo imekuwa ikikutwa na watoto wanaochukuliwa mikoani kwa lengo la kufanyishwa biashara hiyo haramu ya ngono.Binti mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ashura mwenye umri wa miaka 14, akiwa na wenzake wawili, Jenipher na Rose, alikiambia chanzo kuwa, yeye na wenzake  walifika kwenye gesti hiyo kwa kuwa hawana sehemu ya kulala.

“Mimi kwetu ni Ifakara, Morogoro, nimeletwa maeneo haya na mama yangu mdogo, sina pa kulala, nimeona niungane na wenzangu ili nipate pa kulala,” alisema Ashura na kuongeza:
“Mama mdogo aliniambia ili nipate fedha za kujikimu na kulipia chumba lazima niwakubali wanaume wanaokuja hapa kutuchukua kwani siwezi kupata kazi kwa sababu hata shule ya msingi sikumaliza.”

NGONO BUKU MBILI TU!
Alipoulizwa malipo anayopata anapochukuliwa na mwanaume, Ashura alisema:
“Mwanaume mwenye huruma anaweza kukupa pesa nyingi lakini wengi wanatoa buku mbili kwa usiku mmoja na chumba analipia yeye.”
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger