Home » » Yanga kikaangoni Cairo leo

Yanga kikaangoni Cairo leo

Written By Koka Albert on Friday, March 2, 2012 | 11:59 PM


Michael Momburi, Cairo
MABINGWA wa Tanzania, Yanga wanaingia dimbani leo wakiwa na lengo la kuvunja mwiko wa kufungwa na timu za kaskazini watakapoivaa Zamalek kwenye Uwanja wa Chuo cha Jeshi majira ya saa 12 jioni sawa na saa moja usiku za Tanzania.

Katika mechi hii ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inahitaji sare ya mabao 2-2 kusonga mbele au ushindi wowote kutokana na matokeo ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza mjini Dar es Salaam, lakini suluhu au sare ya bao 1-1 ni nzuri kwa Zamalek.

Pamoja na ndoto hiyo wachezaji wa Yanga wanapaswa kusahau hali ya hewa ya baridi ambapo leo inatarajiwa kufika nyuzi joto 13 -14 wakati mechi hiyo itakapokuwa ikichezwa.

Pamoja na hali hiyo kocha wa Yanga, Kostadin Papic leo atalazimika kuendelea kutumia mfumo wake wa 4-3-3 na kuhakisha anapata bao la mapema litakalomwezesha kukaa kwenye mazingira mazuri ya kufuzu.

Hakuna shaka safu ya ushambuliaji wa Yanga itaanza na washambuliaji Davies Mwape, Asamoah na Hamis Kiiza akitokea pembeni huku Jerryson Tegete akiwa benchi.

Kutokana na kelele za mashabiki na viongozi wa Yanga, kocha Papic aanaweza pia akampa Tegete kuthibitisha ubora wake mbele ya ngome ya Zamalek.

Safu ya kiungo itaongozwa na Haruna Niyonzima akipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Nurdin Bakari aliyekuwa majeruhi pamoja na Juma Seif 'Kijiko' katika kuhakikisha wanavuruga mipango yote ya Zamalek.

Kurejea kwa Ahmed Hossam ìMidoî aliyekuwa nje kwa miezi miwili na kiungo Mahmoud Abdul-Razek 'Shikabala' kwa Zamalek kutamlazimisha kocha Papic kutoa mbinu mpya kwa ngome yake.

Nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na beki wa kushoto Stephan Mwasika bado hawaonyeshi kiwango cha kuvutia tangu waliporejea baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Mabeki wa kati Nadir Haroub na Athuman Idd watakuwa na jukumu moja kubwa la kuhakikisha mshambuliaji Razak Omotoyossi na Mido hawachezi mipira yote ya krosi kutoka kwa Shikabala.

Haki za matangazo ya mchezo huo zimenunuliwa na klabu ya Al Ahly mwezi mmoja uliopita uliopita

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger