Home » » Mgomo wa madaktari wanukia tena

Mgomo wa madaktari wanukia tena

Written By Koka Albert on Saturday, March 3, 2012 | 12:03 AM

Geofrey Nyang’oro
MADAKTARI huenda wakagoma tena baada ya kikao kati ya serikali na madaktari hao kuvunjika kutokana na kutokuelewana.
Hali hiyo imejidhihirisha baada ya kutokea kutoelewana baina ya wawakilishi wa madaktari hao na maofisa wa Serikali katika ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mgomo wa awali ulimalizika Februari 8, mwaka huu baada ya Pinda kufanya majadiliano na wawakilishi wa madaktari na kuwaomba warejee kazini, kwa maelekezo ya kushughulikia madai yao.
Mtafaruku huo wa sasa umetokea siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kupitia hotuba yake ya Februari kuwataka madaktari hao kuwa na moyo wa subira na kuendelea kutoa huduma kwa Watanzania wakati Serikali ikishughulikia madai yao.

Mtafaruku huo ulitokea juzi na madaktari hao waliamua kuondoka na kuvunja kikao kilichofanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, kujadili madai yao.

Kumekuwepo na mkanganyiko wa sababu zilizofanya madaktari hao kujiondoa kwenye meza ya mazunguzo baada ya taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba kikao hicho kimevunjika kutokana na pande hizo mbili kutofautiana.

Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa moja ya sababu za kuvunjika kwa kikao hicho ni madaktari kupinga hoja ya kuhusisha makundi mengine kutoka sekta ya afya kama wafamasia na wauguzi.
Lakini Rais wa chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Namala Mkopi aliliambia Mwananchi kuwa wao walikwenda katika ofisi za Waziri Mkuu kufuata majibu ya barua yao waliyoiwasilisha kabla ya mkutano, lakini hawakupewa barua ya majibu.

Alisema barua hiyo pamoja na mambo mengine ilikuwa na maswali kadhaa yanayotaka ofisi hiyo ijibu huku ikieleza namna wao wanavyotaka mkutano wa majadiliano baina yao na Serikali uwe.

“Sisi hatukwenda kukutana kwa ajili ya majadiliano na wahusika bali tulifuata majibu ya barua yetu tuliyowasilisha kwao kabla ya mkutano huo, taarifa ya kuwa sisi tulitoka kwenye mkutano kutokana na kukataa makundi mengine ni za uongo na wameamua kufanya propaganda katika hilo, lakini sisi ni watu wazima tunaelewa.

"Acha wao wafanye propaganda, sisi ni watu wazima tunajua itafika wakati tutakaa nao chini na kufanya uamuzi wenye kuzingatia masilahi yetu na ya umma,” alisema Mkopi.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger