Home » » Kesi ya Mpendazoe, Dk. Mahanga kuanza leo

Kesi ya Mpendazoe, Dk. Mahanga kuanza leo

Written By Koka Albert on Thursday, March 1, 2012 | 11:26 PM

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inaanza rasmi kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010, ambapo Dk. Makongoro Mahanga (CCM), alitangazwa kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo la Segerea.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA), Fred Mpendazoe, akidai kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alikiuka taratibu za uchaguzi hivyo anaiomba mahakama itangaze kuwa uchaguzi huo ulikiuka taratibu na sheria ya uchaguzi.
Katika kesi hiyo Mpendazoe anatetewa na wakili wa kujitegemea, Peter Kibatara, wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayetetewa na wakili wa kujitegemea David Kakwaya na Dk. Mahanga anatetewa na wakili wa kujitegemea, Jerome Msemwa.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Ibrahim Juma, imepangwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia leo hadi Aprili 13. Hii inakuwa kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika mkoa wa Dar es Salaam kufikia hatua ya kuanza kusikilizwa.

Novemba mwaka 2010, Mpendazoe kupitia wakili wake Kibatara, aliifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiomba mahakama hiyo itengue matokeo yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mshindi.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger