Home » » Watu sita wafa katika ajali Kibaha

Watu sita wafa katika ajali Kibaha

Written By Koka Albert on Sunday, March 4, 2012 | 9:58 PM

Sanjito Msafiri na Julieth Ngarabali,Kibaha
 WATU SITA wamefariki dunia na wengine 46 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana Kibaha mkoani Pwani. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na polisi zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea saa saba mchana wakati gari mbili za  abiria aina ya Costa moja ikitokea Dar es Salaam na nyingine Mlandizi mkaoni Pwani zilipogongana uso kwa uso katika eneo la Kwabonde.

Kwa mjibu wa mashuhuda ajali hiyo ilitokea baada ya gari moja la abiria lilikuwa likitokea Dar es Saam kwenda Mlandizi lilipojaribu kuyapita magari mengine. Mganga Mkuu wa Hosptali ya Tumbi,  Dk Isaack Lwali alisema alipokea miili sita ya watu walikufa papo hapo na majeruhi 46. Alitaja walioppoteza maisha kuwa ni Hadja Abdallah (26) na mwanaye Abdallah Juma (4)wakazi wa Miemba Saba mjini Kibaha.

 Wengine ni Siwema Ali (26) na Mariamu Ali (6)wakazi wa Tanga, mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Mntenga na mwingine anadaiwa kuwa dereva wa moja ya gari hizo zilizogangana ambaye jina lake halijafahamika. Dk Lwali alifafanua kuwa kati ya majeruhi waliowasilisha hosptalini hapo wanne kati yao wamepelekwa Hosptali ya Taifa ya Muhimbili huku, 42 wakiendelea na matibabu hosptalini hapo.

Kwa upande wake afisa habari wa Polisi Pwani, Insekta Athumani Mtasha ameongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni daladala Toyota costa kuyapita magari mengine na kukutana uso kwa uso na daladala hiyo nyingine na kusababisha vifo na majeruhi hao.

Nao mashuhuda wa ajali hiyo walisema abiria wengi wa ajali hiyo waliumia sana na huenda idadi ya vifo vikaongezeka kutokana na kuwa wengi walishindwa kuokolewa kwenye daladala hizo kutokana na kubanwa ambapo ilichukua muda wa dakika 45 kupatikana ufumbuzi ambapo ililetwa malori mawili kwa ajili ya kuvuta kuyatenganisha.

 Ni siku tano tu zimepita tangu watu  tisa kufarikii dunia na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea kwa nyakati tofauti katika eneo la Mlandizi Kibaha na Ikwiriri Rufiji.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger